VODACOM

Makonda atoa kompyuta 50 sekta ya ardhi

picha na Steven Charles kejo@kejonews.com. MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (pichani) amekabidhi kompyuta 50 ili kuanzisha mfumo wa utoaji vibali vya ujenzi na ardhi kwa njia ya kielektroniki kwa halmshauri sita za jiji la hilo. Akikabidhi kompyuta hizo kwa maofisa ardhi wa halmashauri hizo katika ukumbi wa Anartouglo, Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana, Makonda pia aliahidi kutoa kompyuta 600 kwa watendaji wa serikali za mitaa zitakazowezesha kuunganishwa katika mfumo huo. Makonda alisema anataka kompyuta hizo zitumike kwa ajili ya kuwaondolea changamoto wananchi za upataji vibali vya ujenzi kwa kuwa suala la ufuatiliaji vibali hivyo ilikuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi, hali iliyochangia sekta ya ardhi kugubikwa na vitendo vya rushwa na urasimu Aidha Makonda alitoa kompyuta nane kwa manispaa za mkoa huo pamoja na kompyuta tano kwa

No comments