wanaotoa siri za serikali mtandaoni kutupwa jela miaka 20
Waziri wa nchi, Ofisi ya raisi anayeshughulikia menejimeti ya utuishi wa umma na utawala Bora, Bi Angela Kairuki.
By steven Charles Kejo, Kejo news.com,kejocharles.blogspot.com.
SERIKALI imetoa onyo kwa watumishi wa umma wanaotoa siri za serikali na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa watachukuliwa hatua za kisheria.
Kairuki alisema mtumishi wa umma atayejihusisha na usambazaji wa taarifa za serikali, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufikishwa mahakamani na kupewa kifungo cha miaka 20 jela. Alisema serikali ina utaratibu wake wa kutoa taarifa kwa umma ikiwa ni pamoja na kupitia machapisho yake kwa jamii.

Post a Comment