Wanamuziki na wachezaji matajiri duniani watajwa
Jarida la Forbes limetoa orodha ya watumbuizaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi duniani, Sean "Diddy" Combs ndiye anayeongoza. Mapato yake yalikuwa $130m (£102m), jambo lililomsaidia kupanda sana kutoka nafasi ya 22 mwaka jana. Ufanisi wake unatokana na ziara yake ya majuzi Marekani, mkataba wa mauzo kati yake na kampuni ya vodka na hatua yake ya kuuza nembo yake ya mavazi ya Sean John. Beyonce na JK Rowling wanashikilia nafasi ya pili na ya tatu mtawalia, lakini jambo la kushangaza ni kuwa wanawake katika orodha hiyo ya wasanii na wachezaji 100 ni asilimia 16 pekee. Wanamuziki watano wa Hip Hop matajiri zaidi duniani Walioingia katika orodha hiyo mara ya kwanza mwaka huu ni pamoja na Kylie Jenner, aliye nafasi ya 59. Yeye ndiye wa umri mdogo zaidi katika orodha hiyo, akiwa na miaka 19. Mapato yake yanatokana sana na kipindi cha uigizaji wa maisha ya uhalisi runingani cha familia yake, kipindi cha Keeping Up with the Kardashians. Alipokea mapato pia kutoka kwa kampuni ya manukato na vipodozi ambayo ina jina lake, nembo ya mavazi na pia kushirikishwa katika kutangaza na kuuza bidhaa mbalimbali. Nusu ya walio katika 10 bora ni wanamuziki, lakini kuna wachezaji wawili - Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na nyota wa mpira wa kikapu LeBron James. Hii hapa orodha ya 10 bora:
Post a Comment