GEPF yakikopesha kikundi sh.500 milioni
In short summary..
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa GEPF, Joyce Shahidi na Mwenyekiti wa Sukari Saccos, Pandu Khamis wametiliana sahihi ya mikataba ya mkopo huo leo(Ijumaa).
Mfuko wa pensheni wa GEPF umetoa mkopo wa Sh500 milioni kwa Chama cha Usharika cha Akiba na Mikopo cha Sugar, kilichoundwa na wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha sukari cha Kagera Sugar, kilichopo Kagera. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa GEPF, Joyce Shahidi na Mwenyekiti wa Sukari Saccos, Pandu Khamis wametiliana sahihi ya mikataba ya mkopo huo leo(Ijumaa). Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Khamis amesema mkopo huo wa miaka mitatu utasaidia katika kuongeza ari ya kazi miongoni mwa wanachama. "Mkopo huu utasaidia kuhamasisha wanakikundi ambao ni wafanyakazi wa Kagera Sugar kuwajibika zaidi hivyo kuongeza uzalishaji hali ambayo itawezesha sukari kupatikana kwa wingi nchini na pengine tukapata ya kuuza hata nje ya nchi," amesema mwenyekiti huyo.

Post a Comment