VODACOM

Malinzi,madega wachukua fomu ya uraisi wa TFF utakaofanyika Dodoma

Kuuli alisema kamati yake itafanya kazi na taasisi nyingine za Serikali ikiwemo taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuri) ili kukwepa tuhuma zote za rushwa  Uchaguzi mkuu wa Shirikisho la soka (TFF), umezidi kupamba moto baada ya Rais anayemaliza muda wake Jamali Malinzi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga Imani Madega kuchukua fomu za kugombea nafasi ya urais wa Shirikisho hilo leo Ijumaa Juni 16, 2017. Uchaguzi unatarajia kufanyika Agosti 12, Dodoma kama ilivyotangaza na Wakili Revocatus Kuuli Kuuli alisema kamati yake itafanya kazi na taasisi nyingine za Serikali ikiwemo taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuri) ili kukwepa tuhuma zote za rushwa. "Uchaguzi wa safari hii utakuwa tofauti na wa miaka mingine yote tutakuwa makini na hatutakubali kudanganywa kwa aina yoyote ile na ili atakayepata nafasi ya kushinda katika uchaguzi apate nafasi hiyo kwa uhalali," alisema Kuuli. Katika nafasi ya Umakamu siku ya jumapili Mwenyekiti wa chama cha mpira Dodoma 'DOREFA' Mulamu Ng'ambi naye atakwenda kuchukua fomu ya kugombania nafasi hiyo.

No comments