Meya wa Manispaa ya ubungo apanga mpango wa kuboresha soko la shekilango
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Ubongo, Boniface Jacob amefanya kikao na wafanyabiashara wa Soko la Shekilango ili kuweka makubaliano ya maboresho ya soko hilo.
Maboresho hayo ambayo yamelenga kuliweka soko la Shekilango na masoko mengine ya Manispaa ya Ubongo katika hadhi nzuri na kuongeza mapato kwa serikali.
Akizungumza na wafanyabiashara katika soko hilo, Jacob amesema, maboresho ya soko hilo yametengewa Tsh milioni 50 ambazo ni mapato ya ndani ambayo yaliyotokana na kodi zao. Amesema maboresho hayo yataanza baada ya siku 7, yatachukua siku 14 kukamilika na wafanyabiashara waliopisha marekebisho hayo kurudi sehemu zao za biashara.
Jacob amesema mara baada ya wafanyabiashara kurejea katika maeneo yao, makubaliano ya ushuru yatakuwa baina ya Manispaa ya Ubungo na mfanyabiashara na siyo tena mfanyabiasha na mfanyabiashara.
"Nimekuja kuwasikiliza wafanyabiashara wote sitaki kuwaletea njaa,nataka tuangalie hali ya sasa na mzunguko wa ela tangu 2000 na tukubaliane".
Jacob amesema mara baada ya maboresho ya mabanda ya mbogamboga ambayo ushuru wake utapanda kidogo, awamu itayofuata itawagusa wapanga na wamiliki wa fremu 12 na vyoo ambao kwasasa wanalipa sh 200 kwa siku.
Aidha Jacob aliwataka wamiliki wa fremu hizo kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa kufanya mazungumzo naye ili kupata makubaliano ya pamoja ya kisheria ili fremu hizo ziwe mali ya serikali na wao kulipia ushuru unaoendana na mahitaji ya sasa kiuchumi.
Post a Comment