VODACOM

Moto wa msitu waua watu 25 ureno

HABARI
 By Mwandishi Steven Charles kejo,  kejonews@kejocharles.blodspot.com

SUMMARY
Maofisa wa Ureno wamesema kuwa, moto huo ulianzia katika maeneo ya katikati mwa nchi hiyo na kusababisha vifo hivyo huku watu wengine 20, wakijeruhiwa wakiwamo maafisa kadhaa wa zima moto.Watu zaidi ya 25 wamefariki dunia baada ya moto mkubwa ulioanzia katika msitu ulio karibu na mji wa Pedrogao kuunguza makazi ya watu. Maofisa wa Ureno wamesema kuwa, moto huo ulianzia katika maeneo ya katikati mwa nchi hiyo na kusababisha vifo hivyo huku watu wengine 20, wakijeruhiwa wakiwamo maafisa kadhaa wa zima moto. Awali watu waliofariki walikuwa 19, lakini sasa idadi hiyo imepanda na kufikia 25. Mpaka sasa chanzo kilichosababisha moto huo hakijabainika. Kwa muujibu wa maofisa wa serikali wa nchi hiyo, wengi walifariki wakati wakiukimbia mji wa Pedrogao Grande, kilomita 50 kama (Maili 30) Kusini mashariki mwa Coimbra, kwa kutumia magari yao. Watatu kati yao walifariki baada ya kuvuta hewa yenye moshi mkali. "Hili linaonekana ni janga baya zaidi ambalo tumewahi kushuhudia katika miaka ya hivi karibuni, katika moto wa nyika," amesema Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Antonio Costa. Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo João Gomes, amewaambia waandishi habari kuwa, watu 16 wameteketea ndani ya magari yao hadi kufa, wakati walipojaribu kukabiliana na moto huo mkubwa katika Wilaya ya Pedrógão Grande. “Moto ulienea kwa kasi mno katika maeneo manne,” amesema Gomes. Hispania imetuma ndege mbili zitakazosaidia kuuzima moto huo.

No comments